Adam Ndatulu

Adam Ndatulu

Mtaalam wa Kongani & Ubia - Kongani ya Kilombero

Adam ni Mtaalam wa Ubia katika Kongani ya Kilombero na alijiunga na Taasisi ya SAGCOT mwaka 2016. Ni mhitimu wa Shahada ya Kwanza katika Uchumi wa Maendeleo kutoka Chuo cha Mipango na Maendeleo ya Vijijini (IRDP) jijini Dodoma. Mojawapo ya ujuzi wa msingi alionao ni Uchambuzi wa Sera na Utafiti. Kabla ya kujiunga na Taasisi ya SAGCOT kama Mratibu wa Ubia, Adam alifanya kazi kama Afisa Tathmini & Ufuatiliaji katika Tassisi ya (BRITEN) inayoshughulika na kujenga uwezo wa wanufaikaji kama wakulima wadogo waishio vijijini kujiongezea vipato kupitia ujasiriamali.