Alice Peter

Alice Peter

Mhasibu Msaidizi

Alice ana jukumu kubwa la kushughulikia kazi za kila siku za uhasibu katika Taasisi ya SAGCOT. Anamsaidia Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala vilevile kama Meneja wa Fedha kama jukumu lake. Ni mhitimu wa Shahada ya Kwanza katika Usimamizi wa Biashara yenye ubobezi katika Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Bangalore nchini India na ana Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Cyprus, nchini Cyprus. Alice alianza kufanya kazi ya fani aliyosomea kama Afisa Mtaji Watu Uajiri na kazi za Raslimali Watu katika kampuni ya Deloitte Tanzania. Uzoefu wake unajumuisha kazi za uendeshaji, uajiri, uhasibu – uzoefu alioupata alipokuwa akifanya kazi na kampuni ya Sage Evolution, Paste and Tally 9.0 (ERP), usimamizi wa matukio, uandikaji ripoti na usimamizi wa kanzidata.