Anna Mtaita

Anna Mtaita

Mkuu wa Idara ya Fedha & Utawala

Anna ni Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala na alijiunga na Taasisi ya SAGCOT mwaka 2016. Ni Mtunza fedha na Mtekelezaji wa mifumo na sera za fedha kuhakikisha miongozo/ na taratibu za usimamizi wa fedha na uhasibu zinafuatwa. Pia anasimamia timu ya uhasibu na fedha pamoja na kubeba jukumu la kusimamia raslimali fedha za Taasisi ya SAGCOT na wafadhili. Kabla ya kujiunga na Taasisi ya SAGCOT, Anna alifanya kazi katika Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC), wakala wa serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kama MIdara wa Fedha na Utawala kwa kipindi cha (2015 – 2016). Anna ni mhitimu wa Shahada ya Uzamili Sayansi ya Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde nchini Uingereza na pia ni Mhasibu wa Umma Aliyeidhinishwa mwenye cheti cha uhasibu cha CPA (T) akiwa na uzoefu wa miaka 18 ya kufanya kazi baada ya kuhitimu. Pia ana Stashahada ya Juu ya Uhasibu aliyohitimu kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) nchini Tanzania.