Geoffrey Kirenga

Geoffrey Kirenga

Afisa Mtendaji Mkuu

Kirenga amekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya SAGCOT tangu mwaka 2012??. Ni mhitimu wa Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Elimu ya Wadudu Waharibifu wa Mazao ya Kilimo kutoka Chuo cha Imperial kilichopo Chuo Kikuu cha London na ana uzoefu uliotukuka katika minyororo ya thamani ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki. Alikuwa ni MIdara wa Idara ya Maendeleo ya Mazao ya Kilimo katika Wizara ya Kilimo, Usalama wa chakula na Ushirika. Kabla ya kushika wadhifa huu hapo juu, Kirenga amebobea kwenye huduma za uboreshaji mazao ya kilimo, udhibiti wadudu na kinga ya mimea. Kirenga ana mtandao mpana miongoni mwa jamii zinazojihusisha katika kilimo na kilimo biashara nchini Tanzania na kwenye ngazi ya kimataifa, na ni kiongozi anayejituma kwa kiwango cha juu anayeongoza Mpango wa Kukuza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) kuleta matokeo yanayochangia kufanikisha jukumu la taasisi hii kama kichocheo muhimu kinachochangia mabadiliko kwenye sekta ya Kilimo nchini Tanzania.