Honest Ngowi

Honest Ngowi

.

Marehemu Honest Prosper Ngowi alikuwa ni Profesa wa Uchumi, mtafiti na mtaalam mshauri wa Uchumi na Biashara katika Chuo Kikuu cha Mzumbe. Alikuwa ni Mkuu wa Idara ya Kozi za Muda Mfupi, Utafiti na Utaalam Ushauri. Alikuwa ni mwandishi mahiri aliyeandika na kuchapisha kwa upana (zaidi ya machapisho ya kitaaluma 70, zaidi ya tafiti 80 na ripoti za utaalam ushauri na zaidi ya makala 50 kwenye magazeti na majarida) katika masuala ya uchumi, biashara na maeneo yanayohusiana na mambo hayo.

Alikuwa ni mjumbe katika bodi tofauti ikiwemo Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Uchumi na Jamii (ESRF), Shirikisho la Vyama vya Kiraia nchini (Mwenyekiti wa Bodi kwa miaka miwili mpaka mwaka 2017), Swiss Aid, Restless Development, Envirocare; Skuli ya Biashara katika Chuo Kikuu cha Stellenborsch nchini Afrika Kusini na Taasisi ya SAGCOT. Profesa Ngowi alikuwa ni mtu mashuhuri katika Kituo cha Stadi za Teknolojia Africa, mwanachama wa Muungano wa Wasomi Waandamizi katika Chuo Kikuu cha Lusaka, Zambia na pia alifanya kazi katika nafasi ya Mtafiti Mwenza Mwandamizi Mualikwa katika Chuo Kikuu cha Bergn, Norway. Alikuwa na uwezo wa kuzungumza kwa ufasaha lugha nyingi kama Kiingereza, Kinorway, Kiswahili na lugha za kazi kwa Kidenmaki na Kiswidishi.