Maria Ijumba

Maria Ijumba

Mkuu wa Kongani & Maendeleo ya Ubia

Maria amejiunga na Taasisi ya SAGCOT (SAGCOT CL) mwaka 2014, na ana rekodi nzuri ya uongozi katika nyanja za kilimobiashara na uzoefu mpana wa kuratibu watendaji walioko sekta za umma na binafsi na kuwezesha majadiliano kuhusu fursa za biashara yanayohusisha wadau wa sekta mbalimbali katika uwanja mpana wa minyororo ya thamani kwenye kilimo. Maria ni mhitimu wa Shahada ya Sayansi ya Mazao kutoka Chuo Kikuu cha Makerere Kampala-Uganda, na Shahada ya Uzamili katika Uzalishaji Mimea kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi-Kenya.

Kabla ya kujiunga na Taasisi ya SAGCOT, alikuwa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Faida Market Link Ltd (www.faidamarketlink.or.tz) kwa kipindi cha miaka tisa (09) kisha baadaye akajiunga na Mradi wa SNV – Asasi ya Maendeleo ya Uholanzi kama Mshauri Mwandamizi – Kilimo – Maendeleo ya Mnyororo wa Thamani kwenye Maziwa, akisimamia mkakati wa maendeleo ngazi ya kitaifa. Pia alifanya kazi ofisi ya FAO – Dar es Salaam kama Afisa Programu wa Taifa, Kilimobiashara; FAO – Programu ya Mifumo ya Chakula Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.