Gaudence Temu

Gaudence Temu

Mjumbe wa Bodi

Bw Temu ni kiongozi wa biashara aliyefanikiwa mwenye rekodi nzuri zaidi ya miaka 20 kuongoza biashara mpaka hatua ya mafanikio. Ana utaalam uliobobea katika maeneo ya sheria, usimamizi kimkakati, kuandaa mipango ya fedha na ufuatiliaji, fidia na usimamizi wa vipaji, usimamizi wa viashiria hatari na utawala wa shirika. Alifanya kazi miaka 22 kama Afisa Mtendaji Mkuu & Katibu wa Shirika wa Kampuni ya Swissport Tanzania Plc., ni kampuni ya kimataifa inayoshughulika uhifadhi na utunzaji mizigo kwenye viwanja vya ndege duniani. Ni muasisi na mwenyekiti wa Bongo Export House Ltd (kampuni binafsi ya Tanzania iliyoanzishwa kukuza kuwezesha usafirishaji wa bidhaa za kilimo kutoka Tanzania kwenda nchi za nje).