Prudence Y. Lugendo

Prudence Y. Lugendo

Mtaalam wa Sera

Prudence Lugendo ni Mtaalam wa Sera wa Taasisi ya SAGCOT. Alijiunga na Taasisi ya SAGCOT mwaka 2018 na ni mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Uchumi Kilimo na Kilimo Biashara, pia ni mhitimu Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Uchumi Kilimo, Shahada zote mbili alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) mjini Morogoro.

Kabla ya kujiunga na Taasisi ya SAGCOT, alifanya kazi kama Mtafiti Msaidizi katika Tassisi ya Utafiti wa masuala ya Uchumi na Jamii (ESRF) na baadaye alijiunga na Chuo cha Kimataifa cha Utafiti wa Kilimo kanda ya Kitropiki (IITA) kama Mchambuzi wa Sera chini ya mradi ulijuolikana kama Jukwaa la Uchambuzi wa Sera za Kilimo na Uratibu (PAPAC) katika Wizara ya Kilimo.

Ana uzoefu mkubwa katika Uchambuzi wa masuala ya Uchumi Mdogo na Mkubwa; Uchambuzi wa Mahesabu ya Kiuchumi; Uchambuzi wa Minyororo ya Thamani kwenye Kilimo; Mabadiliko katika Taswira ya Kilimo; Utafiti wa Sera; Utetezi wa Sera na Tathmini ya Matokeo za Sera. Prudence Lugendo pia ni Mtafiti Mwenza wa Borlaug kutoka Chuo Kikuu cha Nebraska Lincoln (UNL) kuanzia mwezi Septemba mpaka Desemba 2016. Ametayarisha na kutoa machapisho mbalimbali ya utafiti kuhusu uzalishaji kilimo wenye tija ikijumuisha matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri kilimo; matokeo za skimu za umwagiliaji kwa wakulima wadogo kwenye kupunguza umaskini na masoko ya mazao ya kilimo na ana uzoefu wa zaidi ya miaka 8 ya kufanya kazi na Sekta Binafsi na Washirika wa Maendeleo.