Shazdah Sadry

Shazdah Sadry

Msimamizi wa Ofisi na Afisa Mawasiliano - Dar es Salaam

Shazdah ni kiungo muhimu kwenye upande wa utawala katika Taasisi ya SAGCOT akiwa ni Msimamizi wa Ofisi ya Kongani ya Kilombero. Pia anatekeleza jukumu la Msaidizi wa Afisa Mtendaji Mkuu na anasimamia Kitengo cha Mawasiliano ambapo hushughulikia masuala yahusuyo vyombo vya habari kwa jamii na mawasiliano yote ya nje ya nchi na mikutano mbalimbali. Ana uzoefu mkubwa katika Usimamizi wa Ofisi vilevile katika Usimamizi wa Raslimali Watu, akiwa amefanya kazi kwa nafasi kama hiyo aliyonayo sasa katika asasi tofauti zenye kuaminika kama vile Occasions by Jo nchini Kenya, Breakthrough Attorneys, First National Bank na Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC). Alijiunga na Taasisi ya SAGCOT mwezi Mei 2016 na ni mhitimu wa Shahada ya Kwanza katika Usimamizi wa Raslimali Watu aliyohitimu kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU).