Tulalumba Mloge

Tulalumba Mloge

Meneja wa Kongani & Ubia – Kongani ya Mbarali

Tulalumba ni mhitimu wa Shahada ya Uchumi Kilimo na Shahada ya Uzamili ya Utawala katika Uongozi wa Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi Vitendo cha Nuertingen- Geisslingen nchini Ujerumani. Ana uzoefu mpana katika utafiti, uongozi na uratibu miradi. Kabla ya kujiunga na Taasisi ya SAGCOT, alifanya kazi katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani kwenye kitengo cha utawala na usimamizi wa matukio. Amekuwa mfanyakazi katika Taasisi ya SAGCOT tangu mwaka 2014.