Kitovu cha Taarifa cha SAGCOT

Huu ni muundo wa Ukuaji wa Kijani wa Kilimo. Ramani ilibaindi masuala muhimu ya mabadiliko ya tabia nchi, uhifadhi mazingira, na usimamizi wa maliasili kama ni mambo muhimu kwenye mpango wa muda mrefu wa Ukanda juu ya maendeleo ya kiuchumi, japokuwa haitoi mipango ya kina namna ya kushughulikia masuala hayo tajwa hapo juu. Nia ya Muundo wa Uwekezaji kwenye Ukuaji wa Kijani ni kuboresha mkakati wa SAGCOT kuhakikisha kuwa maendeleo katika Ukanda ni endelevu kwa mazingira, yanaleta haki sawa kijamii, na yanaweza kuleta faida za kiuchumi. Mahsusi kabisa, Ramani ya Kijani imeweka mkakati wa utekelezaji wa “Ukuaji wa Kijani wa Kilimo” kuendeleza kuimarisha kilimo kwa wakulima wadogo na wakulima kibiashara, wakati huohuo kwa pamoja wanahifadhi mali asili ambao ni msingi kwa kusaidia kilimo na kupunguza shinikizo kwenye misitu, raslimali maji na bayoanuai.


Bofya Hapa Kupakua Mpango wa Ukuaji wa Kilimo Shirikishi

Kanda za Kilimo Kwanza ni ubia wa kimataifa kati ya Serikali na Sekta binafsi uliozinduliwa kwenye Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani mwezi Mei 2010 jijini Dar es Salaam, Tanzania.  Ubia huu una malaka ya kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi na ubia kusaidia kufanikisha malengo ya Mkakati wa Kilimo Kwanza nchini Tanzania. Kuchochea uwekezaji mkubwa wa sekta binafsi wajibifu, mpango unalenga kuleta ukuaji wa haraka na endelevu wa kilimo, ukiwa na manufaa makubwa kwa usalama wa chakula, kupunguza umaskini, na kupunguza majanga ya mabadiliko ya tabia nchi. Wanachama wa ubia wanawakilisha serikali, biashara za duniani, sekta binafsi nchini Tanzania, wakulima, mashirikisho ya taasisi na taasisi za wafadhili. Inaongozwa na Kamati Tendaji inayoongozwa na uenyekiti wenza wa Wizara ya Kilimo Tanzania, na Makamu wa Rais Mtendaji wa Kampuni ya Unilever (Kanda ya Afrika Kaskazini na Kati). Ubia wa Serikali naSekta binafsi awali ulisisitiza kuwa Kamati Tendaji imetakiwa kuandaa Mpango wa Uwekezaji kwa maendeleo ya ukanda wa SAGCOT. Ripoti iliandaliwa na timu ya wataalamu wabobevu wa kilimobiashara Africa walioungana na kuongozwa na Prorustica and AgDevCo. Ubia wa Kilimo Tanzania unasaidia maendeleo ya mpango huo ambapo ubia huu wa kilimo unafanya kazi kama sekretarieti ya mpango ambapo hutoa msaada wa kiuendeshaji kwa maendeleo ya mpango. Jukwaa la uchumi lilitoa msaada wa lazima , ikiwemo kuitisha mikutano muhimu na kukuza mpango huu kimataifa. Timu ya Wataalam ikiunganisha wadau toka sehemu mbalimbali nchini Tanzania na kimataifa, walipewa kazi ni wengi kuwataja hapa, wakitoa maoni na mawazi yenye thamani kubwa. Taarifa iliyotolewa hapa sio ya kina , japokuwa na sio lazima itegemewe kufanya maamuzi ya kiuwekezaji.


Bofya Hapa Kuona Zaidi