John Nakei

John Nakei

Meneja wa Kongani & Ubia – Kongani ya Kilombero

Alijiunga na Taasisi ya SAGCOT mwaka 2014 kama Mtaalam wa Mazingira na Jamii kuwezesha ushiriki kikamilifu wa ubia kati ya serikali na sekta binafsi ka unaolenga kukuza kilimo shirikishi na endelevu katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania. Amefanya kazi Wizara ya Kilimo kwa miaka sita (6) katika kitengo cha Mazingira akiwa na jukumu la kuhakikisha sera, mipamngo, program na miradi ya sekta ya kilimo inazingatia sheria za uhifadhi na utunzaji wa Mazingira kwa ajili ya Maendeleo endelevu. Ana uzoefu wa kusimamia masuala ya uendelevu wa biashara katika miradi midogo midogo, biashara za kati na biashara kubwa. Vile vile ni mbobezi wa kufanya Ukaguzi wa masuala ya Mazingira na Jamii, Tathmini ya Matokeo za Kimazingira na Kijamii kwenye miradi ya uwekezaji katika kilimo kulingana na sheria zinazosimamia mazingira nchini Tanzania. Ni mhitimu wa Shahada ya Uzamili katika Sera ya Umma kwenye Maendeleo Vijijini.