Idara ya Sera kupitia Mkondo Kazi wa Sera ina wajibu wa kujenga uhusiano wa karibu kwenye Ubia wa SAGCOT, ambao ni Sekta Binafsi na Sekta Binafsi, na muhimu zaidi ni Usimamizi wa Mahusiano wa Wadau wa Sekta ya Umma uko chini ya idara hii. Masuala yote yanayohusu Sera na Sheria yanapelekwa kwenye Idara ya Sera ambapo watendaji wa idara hii wana jukumu la Kuchambua Sera, Utetezi na Uanzishaji wa Ubia Mkakati wa Sera.    Lengo la msingi la Idara ni kuleta maboresho katika vipaumbele vya sera yanayoibuliwa kutoka kwenye ubia mkakati wa sekta binafsi kwa niaba ya serikali, kupanua maarifa sahihi, kupeana uzoefu na kujenga uhusiano imara na wabia mkakati wa kisera ili kushirikiana pamoja kutetea maboresho, kufuatilia utekelezaji wa maboresho hayo na vile vile kuhakikisha wabia wa SAGCOT kutoka Sekta binafsi wanafuata sheria na taratibu za utendaji kazi ndani ya ubia. Idara ya Sera pia inafanya kazi ya kuimarisha hili na pia kuimarisha ushirikiano kati ya sekta mbili ambazo ni sekta ya Serikali na Sekta Binafsi. 
Timu ya Sera inasaidia Wabia Mkakati wa Kisera wanaotoka serikalini na kwa watendaji wasio wa kiserikali wanaohusika na wanaoguswa na michakato ya uundaji sera na utekelezaji wa sera katika ngazi ya taifa na mkoa. Kwa upande mwingine Wabia Mkakati wa Kisera ni Wizara na Wakala wa Sekta za Serikali (wakiwemo mamlaka za udhibiti), Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa na vilevile inajumuisha Watendaji wasio wa Kiserikali, wabia wa sekta binafsi wa Kituo cha SAGCOT na (idara nyingine na vitengo) vya Kituo cha SAGCOT. Idara ya Sera inaongozwa na Mkuu wa Sera akisaidiwa na Meneja Sera na Mtaalamu wawili wa masuala ya sera.