- info@sagcot.co.tz
- +255(0) 22 260 1024
Utaratibu wa Utekelezaji wa Mpango wa SAGCOT
Mpango wa SAGCOT unatekelezwa kupitia Kongani. Kongani ni eneo la kijiografia lenye mkusanyiko wa wadau kwenye minyororo mbalimbali ya thamani. Msingi wa Kongani ni kuonyesha mwingiliano wa kazi za wadau katika eneno husika na mahusiano yaliyopo ili kufanikisha maendeleo ya biashara. Taasisi ya SAGCOT kinafanya kazi ya uwakala mwaminifu wa kuunganisha Wabia kusaidia kazi zao kuwa na ufanisi. Ubia wa SAGCOT unashirikisha makampuni ya kilimo biashara, asasi za wakulima, asasi za kiraia, na wakala mbalimbali wa serikali wakipewa jukumu la pamoja la kuendeleza minyororo ya thamani iliyopewa vipaumbele kwenye miradi ya kilimo. Hivyo, wabia hufanya kazi kutatua vikwazo walivyobaini kwa pamoja.
Aina za ubia zimegawanyika kulingana na minyororo ya thamani ambapo kuna minyororo 9 ya thamani; Soya, Chai, Maziwa, Nyanya, Viazi mviringo, Miwa, Mpunga, Parachichi na Alizeti.
Mazingira ya Ubia wa SAGCOT
Kuwashirikisha wakulima wadogo na kuhakikisha wanazingatia uhifadhi endelevu wa mazingira kwa shughuli wanazofanya;
Kushirikiana na wabia wengine ili kukuza njia inayowaunganisha na kuboresha jitihada za pamoja ndani ya minyororo ya vipaumbele ya thamani;
Kudumisha ushiriki, mawasiliano na msaada kwa Taasisi ya SAGCOT;
Kuchangia kwenye utatuzi wa vikwazo vya kisera na miundombinu; na
Kuchochea ubunifu kwenye utatuzi wa changamoto zikiwemo za kifedha.
Unaweza kuuelezea Mpango wa SAGCOT kama ndoto inayotelezeka. Utekelezai wa ndoto au maono hayo unatokanana na kuwepo Mikakati ya Utekelzaji wa Mpango wa SAGCOT inayotekelezwa kwenye vipindi vya miaka mitano-mitano. Mikakati hiyo, hutumiwa kuandaa mipango kazi ya kila mwaka na kuweka mfumo wa kitaasis ya kuratibu na kutathmini utekelezaji kupitia SAGCOT Centre Ltd.Historia Yetu
Taasisi ya SAGCOT Centre Limited (SCL) kilianzishwa kama kampuni yenye dhamana iliyosajiliwa kisheria mnano mwaka 2011. Kituo hiki hufanya kazi kama wakala mwaminifu na kichocheo cha ubia miongoni mwa asasi wabia kuhuisha mipango inayohusu minyororo ya thamani jumuishi, endelevu na yakinifu kwenye kilimo. Jukumu kubwa la Taasisi ya SAGCOT ni kuwezesha wabia ili kutekeleza kazi za minyororo ya thamani jumuishi, endelevu na yenye faida kibiashara kwenye kilimo katika Ukanda wa SAGCOT. Kituo hiki ni kiunganishi cha watendaji walioko kwenye mfumo mzima wa kiikolojia. Majukumu ya Kituo ni pamoja na:
Kufuatilia hatua za maendeleo ya utekelezaji, kupitia zoezi la ufuatiliaji na tathmini ndani ya ubia, kuhakikisha utekelezaji wa ahadi za wabia na maendeleo wanayoyapata ili kufikia malengo yao;
Kuhimiza na kuwezesha ushiriki endelevu wa sekta binafsi katika kukuza ubia imara;
Kuendeleza maboresho ya sera na sheria ambayo ni muhimu katika kufikia malengo ya SAGCOT;
Kutoa masomo, kutumia njia za upangaji mipango ya Kongani na uwezeshaji wa wabia, na kuwasiliana kwa niaba ya Ubia wa SAGCOT na;
Kukuza ubia wa SAGCOT, na fursa zilizopo ndani ya ubia, kwa hadhira pana na kwa safu ya wabia wa kikanda na kimataifa.