- info@sagcot.co.tz
- +255(0) 22 260 1024
Ubia wa Ukanda wa Kukuza Kilimo kusini mwa Tanzania (SAGCOT) una wajibu wa kubadili sekta ya kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, kwa kuchochea uwekezaji jumuishi na wenye uhifadhi endelevu wa mazingira. Kufanikisha lengo hili kunahitaji mipango na uwekezaji ambao unajali mali asili za Tanzania, mifumo ya kiikolojia na bio anuai; kuendeleza mifumo ya uzalishaji kilimo yenye faida na shughuli za uendeshaji wa minyororo ya thamani ambayo inazingatia uhifadhi endelevu wa mazingira na inayowajibika kwa jamii, kuwezesha jamii juu ya mbinu za matumizi bora ya mali asili zilizopo na kuchukua tahadhari dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi; kutengeneza fursa za kibiashara kwa wakulima wadogo na jamii ambazo zitaruhusu uzalishaji wa mali endelevu; na unaozingatia sheria na viwango vilivyowekwa kuanzia ngazi ya kijamii, kitaifa na kimataifa.
Kikundi cha Kilimo endelevu na jumuishi/shirikishi cha SAGCOT (GRG) ni jukwaa la wadau mbalimbali wanaofanya kazi kama chombo cha ushauri kisichokuwa rasmi katika Taasisi ya SAGCOT katika ngazi za taifa na kongani. GRG inawashirikisha pamoja kundi la wawakilishi wa wadau kutoka serikalini (Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara za Kilimo, Maliasili na Utalii, Elimu, Ujenzi, Ardhi na Maendeleo ya Makazi), sekta binafsi (ikijumuisha wakulima na makampuni), jumuiya za wafadhili (RNE, UNEP), na asasi za kiraia (WWF, CARE International, TNC, IUCN and AWF), pamoja na washauri binafsi wa masuala ya kisayansi. SAGCOT GRG ilianzishwa kusaidia Taasisi ya SAGCOT kuratibu na kufuatilia masuala ya kimazingira katika programu zilizoko kwenye Ubia wa SAGCOT. Kimuundo wa utawala, Kikundi cha GRG kinaongozwa na wenyeviti wenza ambao ni Ofisi ya Makamu wa Rais (inawakilisha Serikali ya Tanzania) na Meza ya Majadiliano ya Maafisa Watendaji Wakuu (CEOrt), inawakilisha sekta binafsi. Katika ngazi ya kongani, Kikundi hiki kinasimamiwa na Katibu Tawala wa Mkoa husika vilevile na wawakilishi kutoka makampuni ya sekta binafsi ndani ya kongani kuhakikisha ajenda ya uendelevu na changamto a katika shughuli zote za kongani za SAGCOT. Wabia wawekezaji wa Sekta za Umma na Binafsi walioko katika kongani sio tu wameungana kwa mujibu wa sheria bali kufanya kazi kwa kufuata sheria zilizoko na pia kuungana kiuweledi kuhimiza ushirikishaji wa wadau kwa namna ambayo ni rafiki kwa mazingira na pia ukuaji wa kilimo endelevu kwa jamii, wakifanya kazi kwa karibu na Taasisi ya SAGCOT. Jitihada hii zinatekelezwa kwa nyenzo ya muhimu inayoitwa Mwongozo wa Ukuaji Shirikishi na Endelevu (Inclsuive Green Growth au IGG tool) ambayo SAGCOT hutumia kusaidia makampuni madogo mpaka makubwa kuelewa nini maana ya ukuaji shirikishi na endelevu na namna gani ya kuingiza katika kazi zao za usimamizi.
Ushauri unaotolewa na Kikundi cha GRG hautoi masharti kwa mbia bali huongozwa na Kanuni ya Kushughulika Mambo Hatarishi, Kanuni ya kumtoza malipo Mharibifu/Mchafuzi wa Mazingira na Kanuni Thabiti za Umoja wa Mataifa zinazosimamia Mazingira. Kusimamia matumizi endelevu na kwa busara mali asili zilizopo na kuhimiza ubunifu kwenye Ukuaji wenye uendelevu. GRG husaidia utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi Mazingira iliyosainiwa mwaka 2004 kwenye mipango endelevu ya muda mrefu (miaka 10-30) kama SAGCOT.
Uanachama wa Kikundi cha Rejea Ukijani huakisi Ubia Shirikishi kati ya Serikali na Sekta Binafsi ambao ni haiba ya SAGCOT. Pia huakisi maslahi tofauti na umahri wa kiufundi vinavyohitajika kusimamia utofauti na ugumu unaojitokeza kwenye uendeshaji. Muundo wa Kikundi Rejea Ukijani umelenga kuwezesha kuwepo na ushiriki mkubwa kwa makundi ya wadau wakuu - Serikali ya Tanzania, jumuiya ya wafadhili, sekta binafsi na asasi za kiraia-huku wakitimiza lengo na kuongeza ufanisi. Wanachama wote ni wabia waliosajiliwa kwenye Ubia wa SAGCOT, ukiondoa wataalamu waliopewa mkataba na Kikundi Rejea Ukijani kutoa huduma mahsusi au utaalamu wao.
Kikundi cha GRG kimepanga kuhakikisha kinaweza kuleta matokeo kwa wakati uliopangwa, huku wakitoa majibu kwa mahitaji yaliyowasilishwa na Taasisi ya SAGCOT. GRG kitahakikisha kuwa wataalamu huru wa masuala ya kiufundi na ushauri wa kisayansi wanapatikana muda wowote wanapohitajika na wanachama. Kwa hiyo Taasisi ya SAGCOT kinahitaji wanachama wa GRG kusambaza taarifa, kuomba ushauri na kupewa maelekezo kutoka jamii pana ya wadau kutoka maeneo wanayotoka. Uanachama katika GRG uko kwa mwaliko wa Taasisi ya SAGCOT na Sekretarieti. Utoaji maamuzi ndani ya Kikundi hichi hufanyika kwa msingi wa maridhiano/au makubaliano ya pamoja.