- info@sagcot.co.tz
- +255(0) 22 260 1024
“Ukweli nimefurahishwa na kazi inayofanywa na Taasisi ya SAGCOT (SCL) na wabia wake. Ninaguswa sana na hali ya uwajibikaji iliyopo ambayo ni chachu ya kuongeza na kupanua mafanikio haya tuliyopata. Nilifahamu, sio tu mafanikio yenu na uwezo zaidi ambao upo ndani ya njia ya utekelezaji wa SAGCOT lakini pia changamoto ambazo Tanzania inakabiliana nazo na namna inavyojiandaa kuleta mafanikio kwenye kilimo biashara, kama sehemu muhimu ya “ukuaji wa Viwanda”. Kwa hivyo basi hii imekuwa ikiniangazia sana. Tulipambana sana kupata idhini ya SAGCOT na tutaendelea kukipigania kituo hiki kwa ajili ya siku zijazo. Na pia kuangalia ni jinsi gani tunaweza kutumia nguvu za ziada ili kuimarisha mafanikio ambayo tayari tunayapata”
“Kazi ya Taasisi ya SAGCOT imetupatia ufahamu mzuri juu ya upana, utofauti na uwezo wa wabia wa SAGCOT. Ilishangaza kuona kwamba wabia wameazimia na kuhakikisha kuwa wanarudisha sehemu ya faida wanayopata kwa jamii zilizopo kwenye maeneo wanakoendesha miradi yao, kwa kuanzisha fursa za uzalishaji vipato (ajira), kuwawezesha wakulima wadogo kupata masoko ya mazao yao, na kusaidia upatikanaji wa riziki kwa majirani wa karibu kupitia uanzishaji wa programu za mafunzo na warsha za ushauri wa kitaalam n.k. Ni ukweli ulio wazi kabisa kuwa Taasisi ya SAGCOT kinajijengea heshima, ambayo kwa kiasi kikubwa imetokana na njia ambayo kituo kinatumia kutekeleza kazi zake kwa utulivu, utashi mkubwa na jumuishi ambayo inakubalika na kufuatwa na wadau walioko kwenye ukanda, tangu awali. Nakuomba uendelee kuisimamia kazi hii nzuri unayofanya wewe pamoja na wafanyakazi wote wa Taasisi ya SAGCOT. Hakuna swali kwa namna tulivyofurahishwa kwa yale tuliyoyaona, na tunatazamia kuendelea kuimarisha ubia wa SAGCOT kwa kipindi cha miezi na miaka ijayo”
“Kwa niaba ya Wakala wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania (TSHTDA), Nampongeza Bw. Geoffrey Kirenga kwa kuandaa safari hii ya kihistoria. Safari hii ya kujifunza imepanua uelewa na ufahamu kwa wengi, sio tu Wabunge bali kwa watanzania wote kwa ujumla, juu ya ukweli kuhusu maendeleo ya zao la chai nchini. Hii inahusu hasa, ukitazama ubia kati ya serikali na sekta binafsi kwenye Mradi wa Njombe. Asanteni !”