Ubia wa SAGCOT unaundwa na Serikali ya Tanzania, Sekta Binafsi, Washirika wa Maendeleo, Asasi za Kiraia na vyama/asasi za wakulima. Kituo cha SAGCOT husaidia wabia wake kuendeleza minyororo ya thamani jumuishi. Wabia wengi wanajiunga na Ubia kama wanachama wa jumla kupata taarifa kwa pamoja na kutafuta fursa za ubua kwa uwekezaji na afua ndani ya ukanda. Wabia walioko kwenye kongani za kipaumbele na ubia mkakati wanaunda uhusiano kutatuta masuala ya minyororo ya thamani na kufungua vikwazo mahsusi vya uwekezaji.
SAGCOT hutoa faida nyingi kwa wabia- muhimu zaidi, fursa ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa maendeleo ya kilimo na kuwa sehemu ya kipekee, mpango wa kubadili matokeo.

NINI KITUO CHA SAGCOT KIFANYE KWA WABIA?

Kama wewe ni mwekezaji uliyepo sasa, sisi:

Tunatoa uwanja wa miradi ya uwekezaji jumuishi na kijani,

Kupanua fursa za uwekezaji, mitandao na maarifa kuhusu njia bora za kiutendaji; na

Kuonyesha vikwazo muhimu vya kisera kwa Serikali ya Tanzania na taasisi husika.

Kama wewe ni Asasi ya Wakulima, sisi:

Kuongeza muunganiko kwenye minyororo ya thamani ya biashara na fursa za masoko kwa wanachama

Kuwezesha miradi ambapo wakulima wanaweza kuboresha upatikanaji wa pembejeo zenye ubora wa juu zaidi, teknolojia na mbinu bora za kilimo; na

Kuchangia kuinua vipato na hali ya maisha kwa wanachama.

Kama wewe ni mwekezaji mwenye uwezo, sisi:

Tunakupa taarifa na upatikanaji wa maarifa,

Kubaini fursa mpya za uwekezaji na wabia; na

Kukutambulisha kwenye mamlaka husika za serikali.

Kama wewe ni Mshirika wa Maendeleo au Asasi ya Kiraia, sisi:

Tunapima athari za shughuli zako kwa kuunganisha shughuli zako kwenye miradi mingi ambayo ni jumuishi na endelevu,

Kutoa njia ya kufikia mfumo wa maendeleo ya kilimo ulio kamilifu na wenye ufanisi kupitia uelewano na wawekezaji binafsi, na

Kutoa fursa ya kutetea masuala muhimu ya sera yanayohusu kubadili taswira ya kilimo.

MANUFAA YA KUWA MBIA WA SAGCOT

Kubadilisha Maarifa na Mitandao

Kushiriki katika mikutano mbalimbali, matukio na warsha za Ubia wa SAGCOT ili kubadilishana uzoefu na njia bora za utendaji;

Kupanua mtandao wako kupitia wabia binafsi 120 wa Kituo cha SAGCOT na wizara, idara na wakala na pia Asasi zisizo za Kiserikali;

Kupata taarifa za kimkakati na fursa za uwekezaji;

Kuweza kuimarisha uwezo kwa ajili ya uwekezaji endelevu na maendeleo kupitia Kikundi cha Rejea Ukijani (GRG) na Nyenzo ya Ukuaji Jumuishi wa Kijani and the Inclusive Green growth (IGG);

Jukwaa la kujadili fursa na changamoto za makundi rika; na

Jaribu mawazo yako na kubakia katika masuala ya sasa hivi yanayokinzana yahusuyo kilimo.

Fursa za Mradi na Utetezi

Kuunganisha na wabia wengine wenye uwezo na kushirikiana kwenye mawazo ya uwekezaji na usanifu mradi;

Kujiunga kwenye mikutano. Dhamira na warsha kutafuta fursa za uwekezaji na miradi; na

Kuchangia katika Utetezi kuhusu masuala mahsusi na mbia binafsi katika minyororo ya thamani  - vikwazo mahsusi na masuala ya jumla ya kisera.

Kwa kuongezea, Kituo cha SAGCOT kinabaini ubia mkakatio ambao:

Unatoa suluhu za minyororo ya thamani na uwekezaji,

Kuitisha umoha wa wabia kuimarisha mahusiano

Kutoa fursa za kupima au kuiga miradi yenye tija ili kukuza athari,

Kutoa matokeo yanayoleta mabadiliko kwa wakulima kwa ajili ya usalama wa chakula na kuboresha hali zao za maisha, na;

Kuonyesha athari chanya za kimazingira.

Kanuni za Ubia

Kila mbia ana wajibu wa kufanya yafuatayo..

Kuwashirikisha wakulima wadogo na kuhakikisha wanapofanya shughuli zao wafuate uhifadhi endelevu wa mazingira

Kushirikiana na wengine kukuza njia shirikishi na kuboresha ushirikiano, Kudumisha ushiriki, mawasiliano, na kusaidia Kituo cha SAGCOT

Kuchangia katika utatuzi wa vikwazo vya kisera na kimiundombinu;

Kuzingatia njia mpya na bunifu za uchangiaji fedha

Unayo nia ya kuwa Mbia?

Zungumza nasi.

Tunataka kufahamu kuhusu vitu unavyopenda, shughuli zako na mawazo gani na raslimali zipi unazoleta kwenye Ubia wa SAGCOT.

Kamilisha kujaza maombi yako.

Wafanyakazi wetu watakusaidia namna ya kuweka kumbukumbu sahihi.

Anza kupanga.

Fanya kazi pamoja nasi kuanzisha mpango wa malengo yako, shughuli na matokeo unayotarajia katika Ukanda wa SAGCOT.