- info@sagcot.co.tz
- +255(0) 22 260 1024
Utekelezaji wa kazi za ubia unafanyika ndani ya kongani; maeneo ya kijiografia yenye mkusanyiko wa wakulima waliothaminiwa wenye mahusiano yanayowaweka pamoja, miradi ya kilimo biashara, watoa huduma wenye uwezo wa kutoa misaada inayoshabihiana (k.m. miundombinu ya usafirishaji, maghala na huduma za kigani) Njia ya kutumia kongani inasaidia watendaji binafsi kuanzisha shughuli za kiuchumi zenye kuleta manufaa kwa jamii na kuimarisha matokeo zinazopatikana.
Wabia wanaunganishwa na dira/maono ya kawaida, utamaduni na imani ili kufikia lengo la muda mrefu ambalo ni ushirikiano utakaosaidia kubadili taswira ya maendeleo ya kilimo nchini Tanzania. Hii hutoa kiungo muhimu kinachohitajika ndani ya ushirikiano wenye mafanikio kati ya taasisi tofauti zinazofanya shughuli anuai za utekelezaji. Utamaduni wa kawaida unaounganisha ubia wa SAGCOT unaopanuka huku ukizingatia Kanuni za Maadili na kuweka Kanuni za Ubia ambazo wabia wote wanapaswa kuzifuata katika kutimiza wajibu wao wa kiutendaji.