Utangulizi

Mpango wa Kukuza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (“SAGCOT”) ni Mpango wa Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi uliobuniwa kuchangamsha maendeleo ya kilimo biashara endelevu kusini mwa Tanzania na kuhakikisha unaleta manufaa ya wazi kwa wakulima wadogo na jamii zao. Hii inaleta pamoja watendaji wa sekta ya biashara na umma, vilevile asasi za ndani na za kimataifa zinazofanya kazi kwenye minyororo ya thamani ya kilimo. Kuwepo kwa mchanganyiko mpana wa taasisi anuani, kila moja ikiwa na malengo yake, na kukubaliana juu ya namna ya kuendesha kazi zao kwa pamoja.

Kanuni za Ubia wa SAGCOT umeweka muundo kwa ajili ya matarajio ya mwenendo wa Ubia, ikiwemo; tunatarajia nini kutoka kwa kila mbia na wabia wanatarajia nini kutoka kwa kila mmoja wao. Asasi zinazoomba kuwa wanachama wa ubia wa SAGCOT wanapaswa kukubaliana na Kanuni hizi.

Ubia wa SAGCOT – Malengo na Muundo

Lengo la Ubia wa SAGCOT ni kuanzisha na kuendeleza awamu mpya ya ukuaji wa kilimo wenye faida nchini Tanzania. Ubia utafanya yafuatayo (a) kutoa muundo usiofungamana kwa mazungumzo na ushirikiano, (b) kuanzisha miradi ya uwekezaji inayoratibiwa, na (c) kukuza tija kwenye uzalishaji, vipato, ajira, usalama wa chakula na lishe. Ubia utawezesha uanzishwaji wa shughuli nyingi muhimu za kilimo biashara katika maeneo yaliyokusudiwa, yenye uwezo mkubwa wa uzalishaji kilimo. Ubia utafanya kazi ili kuhimiza na kuelekeza msaada na uwekezaji wa sekta ya umma na binafsi katika maeneo haya, na kwa mapana zaidi kufanya maboresho katika shughuli za mnyororo wa thamani na mazingira mazingira ya biashara katika ukanda wote  
Ubia wa SAGCOT umeanzishwa kuondoa upendeleo wa maslahi ya muda mfupi kupitia kusaidia wabia kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya muda mrefu kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini Tanzania. t of agricultural development in Tanzania. Wakulima, wadau wa kilimobiashara, serikali ya mtaa na serikali kuu, wanazuoni, asasi za kiraia, mabenki ya biashara na washirika wa kimaendeleo wanafanya kazi pamoja kwa namna ambavyo hawajawahi kutokea kabla; kuanzisha shughuli nyingi muhimu za minyororo ya thamani zinazosimamiwa na waendeshaji wake kikamilifu. Kwa kuboresha mawasiliano na kuaminiana, na kuimarisha mahusiano, wanachama wataendeleza malengo ya pamoja na kushirikiana katika kupanga na kutekeleza aina mpya ya maendeleo ya kilimo. Utekelezaji utasaidiwa na uratibu bunifu wa fedha, maendeleo ya miundombinu iliyolengwa, maelekezo ya kiufundi, mafunzo na kujenga uwezo, na muundo wa ubia unaoratibiwa na Kituo huru cha SAGCOT, ambako kuna ofisi ya Sekretarieti ya Mpango wa SAGCOT.  
Dhana ya ‘ubia’ ni dhana ya ujumla inayofunika njia ya jumla ya SAGCOT. Kazi ya kuratibu na kuwezesha ubia upate msaada na shughuli za maendeleo huangukia kabisa kwenye kituo cha SAGCOT. Vyombo vikuu vya kiutendaji vya Kituo cha SAGCOT ni (i) Bodi ya Wakurugenzi; (ii) Mkutano Mkuu wa Mwaka na  (iii) Kituo cha SAGCOT kinachofanya kazi muda wote kama Sekretarieti kwenye Mpango wa SAGCOT. Bodi ya Kituo cha SAGCOT inateuliwa na Waliojisajili kwenye Kituo cha SAGCOT na inajumuisha wanachama saba; wane kati yao wenye uzoefu wa ndani na wawili wenye uzoefu wa kimataifa na mmoja kutoka taasisi ya sekta ya umma.

Uanachama wa Ubia wa SAGCOT

Ubia utakuwa wazi kwa kundi kubwa la wanachama wenye maslahi katika maendeleo ya ukanda wa Kukuza Kilimo Kusini mwa Tanzania. Asasi au taasisi yoyote inayopenda kuwa mwanachama kwenye Ubia wa SAGCOT itatuma maombi kwenye Kituo cha SAGCOT, na itakubaliwa na Kamati ya tathmini ya ubia kama mwanachama kwenye Ubia. Wanachama hao ni  wafuatao:

 • Idara za Serikali za Mitaa na Serikali Kuu za Tanzania
 • Watendaji binafsi wa ndani wakiwemo asasi za wakulima zilizoko wilayani na kitaifa, makampuni yanayafanya biashara ya pembejeo na mazao, na wanaohifadhi mazao, Wazalishaji na wasindikaji, taasisi za fedha, programu na miradi inayojishughulisha na kilimo, na huduma kutoka sekta binafsi
 • Makampuni ya kimataifa kutoka sekta binafsi
 • Watendaji wa Asasi za Kiraia
 • Washirika wa Maendeleo

Baada ya kusajiliwa, kila mwanachama wa Kituo atapaswa kutii Kanuni za Ubia.

Image

Kazi za Kituo cha SAGCOT

Ili kuongeza thamani ipasavyo muktadha wa Kanuni za ubia wa SAGCOT, ni muhimu kwa wanachama watarajiwa kuelewa kazi ya Kituo cha SAGCOT, taasisi ambayo itasimamia Kanuni za Ubia. Kituo cha SAGCOT ni Sekretarieti ya Mpango wa SAGCOT; na kitaratibu shughuli na miradi ya uwekezaji inayosaidia wakulima wakubwa, wanaoibukia na wakulima wadogo, na kilimo biashara kwenye maeneo yaliyolengwa yenye uwezo wa kuzalisha katika ukanda (yanaitwa “Kongani”). Shughuli zote na uwekezaji utasanifiwa kuwa ni wajibifu kijamii na kimazingira. (tafadhali tembelea http://sagcotswahili.systemax.co.tz/index.php/en/what-we-do/sagcot-clusters/about-clusters )

Kazi maalumu za Kituo cha SAGCOT (SCL) ni:

Kukuza Ubia

Kusaidia na kusimamia Kanuni za Ubia na kusaidia kila mwanachama kuelewa nini wanachotarajia wao, na ni yapi majukumu na wajibu wao yaliyopo kwenye Muundo wa SAGCOT.

Kufuatilia na Kutathmini athari za Ubia

Japokuwa kila mwanachama atakuwa na jukumu la kufuatilia maendeleo yake ndani ya ukanda, Kituo cha SAGCOT kitafuatilia maendeleo ya jumla. Hii itajumuisha idadi, Ujazo/ukubwa na athari za uwekezaji na ukuaji na faida itokanayo uendeshaji kilimo biashara katika ngazi kubwa, ndogo na ya kati katika ukanda. Athari za mazingira na jamii, kupunguza umaskini na majukumu ya wanawake na vijana pia yatafanyiwa tathmini. (Tazama IGG Nyenzo https://sagcot.co.tz/index.php/sagcot-investment-project/#1603184214831-775007fe-98e0 )

Kusaidia wakulima kupitia asasi nyingine

Kupitia wabia wa mnyororo wa thamani, Kituo cha SAGCOT kiliundwa kuwawezesha na kuwaimarisha wakulima wadogo kuelekea kuwezesha kilimo kama biashara na imechangamana na mifumo ya uzalishaji kwa mkulima kwa ajili ya masoko na maendeleo ya minyororo ya thamani.

Kufanya kazi kama wakala mwaminifu kati ya wahusika mbalimbali

Kituo cha SAGCOT kiliundwa kama mbainishaji wabia na mwitishaji, chini ya Utangulizi ambapo asasi nyingi zinajishughulisha tayari katika sekta ya kilimo, wanaweza kunufaika kutoka kwenye uratibu ulioongezeka kuzingatia, kurahisisha na kuzidisha juhudi kuanzisha ushirikiano na athari kubwa zaidi.

.

Kuratibu shughuli zinazohusu Ukanda

Kwa kutoa ushauri wa kitaalam unaoaminika ili kusaidia wabia kupanga, kutekeleza na kufanya marekebisho ya shughuli zao na kuwaunganisha kwa mapana zaidi kwenye shughuli zinazoendelea na zilizopangwa zihusuzo mpango wa SAGCOT.

Kusaidia uwekezaji wa Viwanda vya Bidhaa za Kilimo

Kituo cha SAGCOT kiliundwa kusaidia uwekezaji katika viwanda kwenye sekta ya kilimo, tunafanya kazi na wawekezaji waliopo na wenye uwezo – ikijumuisha wakulima na wajasiriamali wadogo na kati – kubaini na kufahamu fursa za uwekezaji.

Kusaidia kukuza mazingira endelevu imara kwa watendaji katika sekta

Kituo cha SAGCOT kiliundwa kuungana na watunga sera kuimarisha muonekano kwa mahitaji ya mtendaji na kusaidia kubaini maeneo ya vipaumbele vya sera kwa ajili ya maendeleo ya sekta.

Kamati ya Tathmini ya Wabia

Kamati ya Tathmini ya Wabia wa SAGCOT Partner Evaluation Committee (Evaluation Committee) ilianzishwa mnamo mwezi Juni 2014 kurasimisha mchakato wa upangaji wa wabia wanaotarajia na uhakikishe kuwa unalingana kikamilifu na Ubia wa SAGCOT na malengo yake. Kabla ya hapo, usajili wa wabia ulipitishwa na Timu Andamizi ya Uongozi (kwa mwaka 2013) na kamati tendaji ya Bodi na Kilimo Kwanza (2011-2012). Ilibainika kuwa kulikuwepo na ushiriki mdogo wa watathmini waliokuwa na uzoefu katika kuwezesha uwekezaji, ushiriki wa sekta binafsi na changamoto za mazingira endelevu. Kwa hiyo, ilipendekezwa kwamba Kituo cha SAGCOT lazima kiwe na watathmini toka nje ya kituo katika Kamati hii. Tangu mwaka 2017, Kamati ya Tathmini ya Wabia imekuwa na wajibu wa kusajiri wabia wenye uwezo, kufuatilia maendeleo ya ubia na kuwaindoa wabia ambao hawazingatii Kanuni za ubia kama ilivyoekezwa kwenye nyaraka hii. Kwa kuongeza zaidi, Kamati hupitisha mkakati wa mwaka wa kusajili wabia, ukiangalia mahitaji ya ubia. Kituo cha SAGCOT kinafanya kazi Skama sekretarieti katika Kamati hii, na kuongeza jukumu la kuwatambulisha wabia wenye uwezo kwenye Kamati. Wanachama wa Ubia wa SAGCOT wanategemewa kufanya kazi kama mabalozi wa Ubia wote wa SAGCOT na malengo yake, kutoa msaada kwa wanachama wengine kama inavyofaa, na kupendekeza wanachama wa nyongeza wenye umahiri kawenye Ubia wa SAGCOT kila inapowezekana.

Kanuni za Uanachama

Kila mwanachama wa Ubia wa SAGCOT wanapaswa kuzingatia Kanuni za Ubia:

Makubaliano kuzingatia mbinu mpya na bunifu za kifedha

Ambazo zimelenga kuchochea uwekezaji wa ziada wa sekta binafsi katika ukanda wa SAGCOT kwa njia ambazo zinahakikisha manufaa makubwa pia yanapatikana kwa wakulima wadogo. Hii inahitaji uwekezaji wenye ubunifu, na Utayari wa wakulima na watendaji wa biashara kilimo kukubali aina mpya ya hatari na marekebisho kwa njia wa mazoea ya kufanya kazi kwa mfumo wa jadi.

Makubaliano kuchangia katika utatuzi wa vikwazo vya sera na miundombinu

Kwa kuleta umakini katika Kituo cha SAGCOT ambao utasaidia kushughulikia masuala yanawapa wasiwasi kuhusu mambo mahsusi ambayo kwa sasa yanakwamisha maendeleo ya kilimo biashara katika ngazi ya ndani na kitaifa. Wanachama katika ngazi zote lazima wajiandae na kuweza kuchangia kubaini  na kutoa njia za utatuzi wa vikwazo hivi kila mmoja kulingana na jukumu na wajibu alionao.

Makubaliano kuhusu kuzingatia Kanuni za Ukuaji wa Kijani

(kupata nyenzo za kukuongoza, tafadhali tembelea http://sagcot.co.tz/index.php/mdocuments-library/)

Makubaliano kuhusu Malengo ya jumla ya SAGCOT

Kugawana malengo ya SAGCOT kwa ajili wa ukuaji wajibifu wa biashara pamoja na chakula na usalama wa lishe. Hii inahusisha hitaji la biashara za kilimo zenye kuleta faida kushirikisha wakulima wanaoibuka na wadogo na maslahi yao katika masuala yao ya kiuendeshaji.

Makubaliano kushirikisha ubia, kudumisha mawasiliano na kusaidia Kituo cha SAGCOT

Kusaidia Kituo cha SAGCOT na kazi zake, Mpaka Ifikapo muda ambapo manufaa yataweza kushuhudiwa, na uaminifu wa msingi na wema wa ndani kwa kila mwanachama utakuwa ni muhimu Kudumisha mafanikio.

Makubaliano kufanya kazi na wanachama wengine kukuza mkakati na njia ya ushirkiano

Kiasi kwamba ndani ya nyanja za shughuli zao, kilas mwanachama atashirikiana kwa ujumla, katika mpango ulioratibiwa wa SAGCOT katika kupanga, uwekezaji na sera.

Mikutano ya Ubia wa SAGCOT

Wabia wataalikwa na watapaswa kujisajili na kuwa wanachama wa Mnyororo wa Thamani wa Kimkakati au Ubia wa Kimaudhui (maudhui kama vile Afya ya Udongo, Fedha, Ukuaji wa Kijani). Hizi ni ubia mikakati wenye athari kubwa ndani ya Ubia mkubwa wa SAGCOT ndani yake watendaji walioko mnyororo wa thamani wanaotumia pamoja taarifa, masuala mahsusi kuhusu mnyororo wa thamani, mambo ya kujifunza na fursa, na mahali ambapo kila mwanachama hutoa mrejesho muhimu katika Kituo cha SAGCOT. Wanachama watajiunga kulingana na Hadidu za Rejea walizokubaliana; kupanga pamoja kwa kipindi cha mwaka mmoja juu ya masuala na kutatua kwa pamoja, kukubaliana kupitia/kurekebisha mpango wao mara kwa mara. Ubia mkakati unakutana katika Ngazi ya Kongani; japokuwa, masuala mahsusi ya kisera na udhibiti yanayoibuliwa hapa hupelekwa kwenda kwa wadau/taasisi muhimu za serikali (pamoja na njia nyingine sahihi) kuhusiana na mazingira ya biashara na vikwazo kwenye uwekezaji wa kibiashara katika mnyororo wa thamani, kutafuta na kubaini njia ambazo zitasaidia kutatua changamoto hizi. Masuala mengine na maendeleo yanajadiliwa katika Mikutano ya
Tathmini katika Kongani ambapo maendeleo na masuala ya vipaumbele vya minyororo ya thamani yanajadiliwa kupitia ushiriki mpana wa ubia wa sekta ya umma na binafsi kwa kuwekeana saini na kutathmini kwa kipindi cha mwaka mmoja KOMPAKTI ya Kongani. Wanachama wote wa ubia mkakati wanapaswa kuwa ni waweka saini kwenye KOMPAKTI ya Kongani.

Matarajio ya Wabia kutoka Kituo cha SAGCOT

Wanachama wanaojisajili kwenye Kanuni za Ubia na kulipa ada ya ubia (tazama Kifungu 9) wataweza kupata kwa ukamilifu taarifa, kutandaa, huduma za kitaalam na fursa nyingine kama zinavyotolewa au kuwakilishwa na Kituo cha SAGCOT. Manufaa mahsusi kwa wanachama wa Ubia wa SAGCOT yatajumuisha:

Wakulima na Asasi za Wakulima

 • Kuboresha miunganiko yao na wadau wa kilimo biashara
 • Kupata taarifa juu ya mbinu sahihi za kilimo kupongeza tija kwenye uzalishaji na umahiri, na kupata wasaa wa kukutana na msaada wa huduma mahsusi kila wanapohitaji
 • Kuunganishwa kwenye mifumo iliyoboreshwa ya masoko na fedha
 • Fursa za kuunganishwa na wakulima wengine – wakiwemo wakulima wakubwa na wadogo

Wabia wafadhili

 • Utambuzi wa maeneo yaliyolengwa na shughuli kwa ajili ya programu zilizoratibiwa kuimarisha maendeleo ya sekta binafsi ambayo yanasaidia kuwaunganisha wakulima wadogo
 • Kuweza kupata Uchambuzi na mrejesho juu ya sera ya kipaumbele, udhibiti, bajeti na vikwazo ambavyo vinavyokwamisha faida ya uzalishaji kilimo na uwekezaji wa sekta binafsi
 • Utambuzi wa maeneo ya kuwekeza kwa jili ya kuboresha usimamizi wa mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kusaidia wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum

Serikali za Mitaa na Kuu

 • Utambuzi wa maeneo ya kipaumbele na yaliyolengwa kwa uwekezaji wa umma kuimarisha kilimo biashara
 • Utambuzi wa mahitaji ya vipaumbele kwenye miundombinu
 • Kuweza kupata Uchambuzi na mrejesho juu ya sera ya kipaumbele, udhibiti, bajeti na vikwazo ambavyo vinavyokwamisha faida ya uzalishaji kilimo na uwekezaji wa sekta binafsi
 • Mrejesho wa mapendekezo ya kivitendo juu ya namna ya kuboresha mazingira ya biashara kwa ukuaji wa kilimo

Tassisi za Fedha na Mifuko ya Maendeleo kutoka Sekta binafsi

 • Kutambulishwa kwenye maeneo ambayo shughuli nyingi za kilimo biashara zinaendelezwa
 • Utambuzi wa fursa za kibiashara na wateja wenye uwezo wanaohitaji mikopo/ruzuku ya kifedha kwa muda mfupi na mrefu
 • Muongozo kwenye maeneo ambayo huduma mtambuka za fedha kama ruzuku zinazolingana na vyombo vingine zinatakiwa
 • Kupunguza gharama za miamala kutokana na uwepo wa taarifa za awali na uchambuzi

Miradi ya kilimo biashara ya ndani na kimataifa

 • Kuwezesha upatikanaji wa uhakika wa fedha
 • Uratibu wa maendeleo ya miundombinu kusaidia uwekezaji wa kibiashara
 • Kuwafikia na kupanua wigo wa wateja wenye uwezo
 • Kusaidia kuboresha mazingira ya biashara yanayofaa kwa kilimo
 • Kupata Uchambuzi wa masuala ya minyororo ya thamani
 • Kuunganishwa na makampuni mtambuka na fursa mpya za ubia unaolenga kugawana mazingira hatari.

Asasi za Kiraia/Zisizo za Kiserikali

 • Utambuzi wa maeneo kuweza kutoa huduma zao mahsusi na kusaidia pale ambapo shughuli mtambuka tayari zinaendelea
 • Ushiriki katika majadiliano muhimu kuhusu masuala muhimu ya kisera na udhibiti
 • Fursa za kuunganishwa na kuongeza thamani shughuli za kilimo biashara zinazoendeshwa kwenye kongani

Malalamiko na Migogoro

Endapo wanachama wa ubia wana malalamiko au wasiwasi mkubwa kuhusu matendo ya Kituo cha SAGCOT au namna ambavyo kinaendesha shughuli zake, wanaweza kusajili rasmi malalamiko yao kwa maandishi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha SAGCOT. Yatajadiliwa kwenye kikao kinachofuata cha Bodi kutafuta ufumbuzi sahihi, Njia nyingine ni kusajili malalamiko yao kupitia  http://sagcot.co.tz/index.php/grm/#1527193282350-12fb1456-1660

Ubia na Ada

Uanachama wa Ubia wa SAGCOT Partnership, unaotakana na kutuma maombi kwenda Kituo cha SAGCOT, unalipiwa ada ya mwaka kulingana na hadhi ya taasisi. Uananchama, unaopitishwa na Kamati ya Tathmini ya Ubia, itatoa ushiriki kwenye mikutano ya Ubia wa SAGCOT na kupata taarifa ya shughuli za SAGCOT lkama vile kikosi kazi, kupata tarifa na mikutano

Nia ya ada ya ubia ni kuhakikisha kuwa zile taasisi pekee ambazo zimeonyesha kujali, kujituma zinajiunga na ubia kupitia Kituo cha SAGCOT. Ada zitalipwa kwenye Kituo cha SAGCOT na kutumika kwenye shughuli mahsusi kama vile shughuli za ubia wa SAGCOT.
The following partnership fee scales will be applied:

Aina ya Shirika

Ada ya Mwaka

Makampuni Makubwa (Faida ya Jumla > Dola milioni 5)

TZS 4,000,000

Makampuni ya Kati (Dola milioni 1(Faida ya Jumla Zaidi ya Dola milioni 5)

TZS 1,000,000

Makampuni Madogo (Faida ya Jumla (Dola milioni 1), Washirika wa Maendeleo, Asasi za Utafiti, Asasi za Kiraia CSOs na Wakala au Taasisi za Serikali

TZS 250,000

Vyama vya Wakulima

TZS 50,000

Washirika wa Maendeleo, pamoja na Wizara za Serikali, Wabia wa Maarifa na Taaluma watakuwa wanachama wa Ubia, japokuwa kulingana na michango yao mikubwa kwenye uchangiaji fedha za kuendesha Kituo cha SAGCOT na/ aqu ndani ya ukanda pekee hatutegemi walipe ada ya uanachama. Ada zote zinafanyiwa marekebisho kila mwaka kuanzia tarehe 1 Januari. Kutolipa ada katika kipindi cha miaka matatu mfululizo kutasababisha mwanachama afungiwe kisha kufutwa kabisa.

Mahusiano ya Umma

 • Asasi zote ambazo ni wanachama zinakubali kuwa Uanachama wao kwenye Ubia wa SAGCOT unaweza kutangazwa na Kituo cha SAGCOT kwa njia sahihi za mawasiliano ikijumuisha Tovuti ya Kituo cha SAGCOT.
 • Kituo cha SAGCOT hakitatoa maelezo maelezo ya mawasiliano kwa mtu mwingine yoyote yule bila idhini ya mwanachama
 • Hakuna mwanachama atakayedai kuwakilisha Ubia wa SAGCOT bila maelezo ya makubaliano ya Kituo cha SAGCOT

Wajibu wa Kijamii & Kimaadili

 • Wanachama ni marufuku kuharibu moja kwa moja, au sio sio moja kwa moja kwa makusudi heshima ya kiuweledi, mafanikio au biashara ya SAGCOT.

Kushindwa kuzingatia Kanuni hizi za Uanachama

 • Tendo lolote la kuvunja au kukiuka Kanuni hizi lazima lipelekwe kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha SAGCOT.
 • Ubia wa SAGCOT kupitia Kituo cha SAGCOT, huhifadhi chaguo kufuta Uanachama kwa makosa makubwa ya uvunjaji wa Kanuni hizi bila ya kurudisha ada ya uananchama zilizolipwa kulingana na maamuzi ya wanachama wengi walioko kwenye Kamati ya Tathmini ya Ubia.
 • Kushindwa kulipa ada ya mwaka ya Uanachama kunatatfsiriwa kama ni kuvunja Kanuni za Ubia wa SAGCOT na utaanzisha ukaguzi wa uhusiano/ubia na Kamati ya tathmini kupitia na kutathmini kama afungiwe au asifungiwe  msaada wa kuwezesha uwekezaji kwa mbia mpaka muda wa malipo ya ada ya mwaka ya uanachama.