Kongani ya Ihemi ilikuwa ni ya kwanza kupewa kipaumbele kati ya Kongani sita zilizobainisha katika Ukanda wa SAGCOT ikiwa na fursa nyingi za kilimo biashara na mtandao watendaji. Kongani hii ina uwezo wa kuzalisha mazao ya chakula kwa kipindi cha misimu yoyote. Kongani ya SAGCOT Ihemi inaambaa pande zote mbili za barabara kuu ya Dar es Salaam-Mbeya na imepanuka takriban kilomita 60 upande wa kaskazini na kusini mwa barabara hii. Kongani imechukua maeneo yote ya Mikoa ya Iringa na Njombe. Aina ya biashara  zinazofanyika kwa wabia wa SAGCOT zinahusisha mazao ya  Viazi Mviringo, Soya,ufugaji mifugo, nyanya, parachichi, chai na alizeti.

 Kongani hii inakadiriwa kuwa na idadi ya watu 1,643,335 (2012). Kongani ya Ihemi ina kubwa wa eneo la jumla la kilomita za mraba zaidi ya 60,000. Ni eneo ambalo kilimo ndiyo shughuli ya msingi na husifika kuwa ni eneo la pili lenye pato ghafi la juu zaidi la nchini Tanzania
Image
Image