- info@sagcot.co.tz
- +255(0) 22 260 1024
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mpango wa SAGCOT ni mkutano wa wanachama wote wa taasisi pia ni kikao cha juu cha maamuzi katika hairakia ya mpango. Mkutano Mkuu unajumuisha taasisi tatu waasisi ambazo ni Baraza la Kilimo Tanzania (ACT), Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI). Taasisi hizi ni makampuni yenye hisa katika Mpango wa SAGCOT.
Baraza la Kilimo Tanzania (ACT)
Baraza la Kilimo la Tanzania (ACT) mwamvuli wa Asasi za Sekta Binafsi unaofanya kazi ya ushawishi na utetezi kwa niaba ya wanachama wake katika ngazi ya taifa na ngazi ya chini kuhusu masuala ya sera na mazingira ya biashara yanayoathiri sekta ya kilimo. Lengo la msingi la Baraza la Kilimo Tanzania ni kuunganisha wanachama wote ambao ni jamii ya wakulima na wafugaji nchini Tanzania na kufanya kama chombo cha wanachama katika majadiliano na serikali na vyombo vingine kuhusiana na uundaji na usimamizi wa sera na programu zinazohusika na maendeleo ya kilimo na kilimo biashara nchini. Baraza hili linaundwa na vyama vya wakulima, vyama vya wafugaji, vyama vya ushirika, vyama vya wasambazaji pembejeo, vyama vya wasindikaji wa bidhaa za kilimo, vyama vya wasafirishaji, na watafiti.