- info@sagcot.co.tz
- +255(0) 22 260 1024
Kongani ya Kilombero inajumuisha mkoa wa Morogoro. Ni mojawapo ya Kongani sita zilizobainishwa katika Ramani ya Mpango wa SAGCOT na ni miongoni mwa kongani za awali tatu zilizopewa kipaumbele kwa kipindi cha sasa. Kongani imebahatika kuwa na fursa nyingi za kilimo biashara na vilevile kuwa na mtandao wa watendaji kwenye minyororo mingi ya thamani. Ikiwa na tabia nchi na hali ya hewa na anuai nzuri, ikiwemo hali ya ukame na nusu ukame mpaka hali ya baridi kiasi (mf. maeneo ya milimani ya Matombo na Gairo). Ukiunganisha mito mingi na maeneo yenye ardhi oevu, hii ina maana kuwa na shughuli na kilimo zinaweza kufanyika kwa kipindi cha mwaka mzima katika Kongani ya Kilombero. Maeneo yenye udongo wenye rutuba nzuri katika Bonde la Kilombero yanafaa sana kwa kwa kilimo cha mpungana mazao mengine ya nafaka kwa kilimo cha kujikimu na kilimo cha biashara. Vilevile, wafugaji wametumia fursa ya uwepo wa hali nzuri ya hewa na tabia nchi kuendesha shughuli za ufugaji mifugo katika kongani, wakifuga zaidi mifugo ya kienyeji. Sababu hizi zinaashiria uwezo mkubwa kwa maendeleo na kuwavutia wadau mbalimbali wenye nia kutoka sekta binafsi na watoa huduma wasiolenga kupata faida ambao tayari wameshaunda mtandao wa ushirikiano kwa kuwa wameshabaini fursa mbalimbali na kuzitumia. Watendaji muhimu wa asasi zisizo za kiserikali walio tayari kufanya kazi katika eneo hili wamejikita kwenye usimamizi wa mazingira na uhifadhi wa bao anuai wakati wengine wamejikita kwenye haki za jamii na usimamizi wa ardhi. Jukumu kubwa la serikali katika suala hili ni kusimamia mwingiliano kwenye sekta zote za maendeleo.
Kongani ina Halmashauri za Wilaya tisa, ambazo ni Kilombero, Mlimba, Malinyi, Ulanga, Mvomero, Gairo, Kilosa, Morogoro na Manispaa ya Morogoro. Kwa nyongeza, Kilombero ni nyumbani kwa eneo la Ramsar (ni eneo la ardhi oevu linalotambuliwa kimataifa kwa umuhimu – vilevile Eneo Muhimu la Wanyama aina ya Ndege). Pia ni nyumbani kwa maeneo muhimu ya maliasili na maeneo ya uhifadhi kama vile Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na Mlima Udzungwa, Mlima Uluguru na Hifadhi ya Taifa ya Mwalimu Nyerere (zamani ilijulikana kama Pori la Akiba la Selous). Kutokana na uanuai wa maliasili na mwingiliano wa shughuli za kijamii na kiuchumi ,SAGCOT na wabia wake wanazingatia Kongani ya Kilombero kama ni eneo muhimu kwa maendeleo endelevu ya mkoa na kuna haja ya kuliendeleza katika namna ya “uendelevu ”. Kuwezesha kufanikisha lengo hili, SAGCOT imeanzisha jukwaa la wadau mbalimbali katika ngazi ya ukanda lijulikanalo kama Kikundi Rejea Uendelevu (GRG) kukuza na kufuatilia ukuaji endelevu katika kongani ukiunganishwa kwenye Ubia wa SAGCOT.