Kongani za SAGCOT ni maeneo ya kijiografia yenye mkusanyiko wa makampuni yaliyounganishwa, wazabuni wabobezi, watoa huduma na taasisi zinazoshirikiana. Kongani hizi ambazo zinazolenga hasa kilimo biashara ni maeneo yenye mkusanyiko wa watendaji (kwenye maeneo mahsusi ya nchi hii) wanaoshughulika na uzalishaji, usindikaji, masoko, usambazaji pembejeo vilevile utoaji wa huduma; unaounganisha wawekezaji mbalimbali wanaonufaisha wakulima wadogo, wa kati na wakubwa. Uwepo wa shughuli za kiuchumi zinazoleta manufaa kwa jamii, wakulima, miradi ya kilimo biashara na watoa huduma wanafanya kazi kwa mafanikio kupitia minyororo ya thamani na mikakati ya kimaudhui kufungua fursa za uwezo ndani ya aina za ubia kimkakati wenye maudhui.

Kuna Kongani sita zinazolenga kilimo biashara, nazo ni: Rufiji, Kilombero, Ihemi, Mbarali, Ludewa and Sumbawanga. Kongani ya Ihemi ndio iliyokuwa ya kwanza kuanzishwa ikifuatiwa na Kongani ya Mbarali. Mwaka 2019 ilizinduliwa Kongani ya Kilombero japo utekelezaji wa kazi ukaanza 2020 kwa sababu mbalimbali ikiwemo uwepo wa UVIKO-19. Kongani tatu zilizobakia zitaendelezwa kwa awamu baada ya kuona shughuli za kilimo biashara zinazoendelea kwenye Kongani tatu za Ihemi, Kilombero na Mbarali zimefanikiwa kuleta matokeo matokeo mazuri na masuala ya kujifunza ili tuweze kuyatekeleza kwenye Kongani hizi tatu zilizobaki.

 

Image
Jukumu la Taasisi ya SAGCOT kwenye Kongani ni kujikita zaidi na uundaji wa ubia miongoni mwa wabia wanaojishughulisha na kilimo biashara ndani ya Ubia Mkakati wa SAGCOT. Kwa hiyo Taasisi ya SAGCOT kinawezesha wabia kutekeleza kazi za minyororo ya thamani ya kilimo ambayo ni jumuishi, endelevu na yenye kuleta faida za kibiashara katika Ukanda wa SAGCOT. Maendeleo ya Kongani yanapewa umuhimu mkubwa katika mafanikio ya SAGCOT. Kwenye kongani, watendaji wanapata huduma na faida ambazo wasingeweza kuzipata endapo wangeendelea kufanya kazi kwa kujitenga kwenye eneo husika au bila ya kuwepo ushirikiano na wadau wengine (ndani ya ubia mkakati). Hii inaonyesha nguvu za Kongani hizi zinatoka kwenye ngazi ya ushirikiano kuliko uwezo asilia wa eneo husika uliokuwepo awali.

Majukumu na Kazi za Kongani za SAGCOT

Majukumu mapana na kazi vimegawanywa miongoni mwa wabia mbalimbali walioko ndani ya Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi chini ya Mpango wa SAGCOT na kuelezewa kwa ufupi kama ifuatavyo

Makampuni Binafsi:- Kuanzisha biashara, mazao au huduma zinazotolewa ndani ya Kongani na matokeo yaliyopatikana (kiasi cha uwekezaji uliofanyika, wakulima waliofikiwa, ajira zilizotengenezwa, kiwango cha mauzo, teknolojia mpya zilizotumika, uwezo wa wakulima au viwanda na hekta za ardhi zilizotwaliwa ikijumuishwa na ukuaji endelevu )
Serikali (Serikali za Mitaa na Serikali Kuu):– Kuboresha mazingira ya biashara ukijumuisha vikwazo vya kisera vilivyoshughulikiwa na miradi ya miundombinu, kuhakikisha uzingatiaji sheria- ikijumuisha kufuata kanuni za ukuaji endelevu .
Watendaji wasio wa Kiserikali:– Wanafanya kazi gani kusaidia ajenda ya SAGCOT: Utekelezaji Mradi, uchechemuzi/utetezi ikijumuisha ukuaji endelevu (masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira)
Taasisi ya SAGCOT (Wakala Mwaminifu):- Kuwezesha uwekezaji mbalimbali na kuratibu wadau ndani ya Kongani na kuchochea mahusiano na viunganishi biashara, kuhimiza ushirikiano miongoni mwa wabia
Asasi za Wakulima:– Wasiochukua tahadhari zaidi kwenye kilimo. Wazalishaji wanaolisha wabia wengine wote. Wao ndio walengwa wakuu wa Mpango wa SAGCOT unaohitaji kuwasaidia ili kufanikisha azma ya kubadili kwa upana mkubwa taswira ya kilimo hapa nchini. (Wakulima wanaoibuka) wanazingatia miitikio na kuchukua hatua na kuzielekeza kwenye jitihada za Serikali za Mitaa, Watendaji wasio wa Kiserikali, na Makampuni Binafsi.
Washirika wa Kimaendeleo na Serikali ya Tanzania:- Kutoa msaada wa kifedha kwa kusaidia kusukuma mabadiliko ya kimaono, kusaidia utafiti na mbinu mpya za ubunifu, kujenga uwezo wa watendaji ikijumuisha ukuaji endelevu .