Lilian Lugola

Lilian Lugola

Msimamizi wa Ofisi – Kongani ya Ihemi

Lilian Lugola alijiunga na Taasisi ya SAGCOT mwaka 2016 kama Msimamizi wa Ofisi Kongani ya Ihemi. Ni mhitimu wa Diploma ya Juu katika Utawala wa Biashara kutoka Chuo cha Menejimenti cha Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI) na Diploma katika Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia. Kabla ya kujiunga na Taasisi ya SAGCOT, Lilian alifanya kazi kama Msimamizi wa Ofisi katika asasi ya JHPIEGO na pia katika Nafasi kama hiyo kwenye taasisi ya World Vision. Alifanya kazi kama Mwakilishi wa Huduma kwa Wateja kampuni ya Airtel Tanzania baada ya kufanya kazi pia kama Afisa Tawala kwenye kampuni ya Oceanic Bay Hotel and Resorts. Kabla ya hapo, Lilian alikuwa ni Mratibu wa Uendeshaji katika kampuni ya iWay Africa. Ni mbobevu kwenye maeneo ya huduma kwa jamii, usimamizi na uendeshaji.