Silvanus Mruma

Silvanus Mruma

Mtaalam mshauri wa Ufuatiliaji, Tathmini, Uwajibikaji & Ujifunzaji (MEAL)

Mruma ni mshauri na meneja wa programu mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20, ikiwemo miaka 10 ya kujihusisha na kazi za utaalam ushauri kwenye programu za kuendeleza mifumo ya masoko kwa bidhaa za kilimo cha matunda na mbogamboga, mafuta ya kula, maziwa, nyama nyekundu na nafaka.

Kabla ya kujiunga na Taasisi ya SAGCOT, aliwahi kuwa MIdara wa Mifumo ya Pembejeo na Tija kwenye Uzalishaji wa USAID NAFAKA – Mradi wa Maendeleo Mifumo ya Masoko ya Nafaka (CMSD), ambapo aliongoza kazi mbalimbali za mradi ikiwemo mipango ya kuimarisha huduma kwa wakulima maili ya mwisho kwa kipindi cha miaka saba (2014-2021). Kabla ya kujiunga na mradi wa NAFAKA kipindi cha miaka (2008-2014), alifanya kazi na SNV Tanzania-Taasisi ya Maendeleo ya Uholanzi kama Mshauri katika Maendeleo ya Sekta Binafsi kwa kipindi cha miaka sita (2008-2014) akibobea kwenye minyororo ya thamani ya kilimo cha mbogamboga na matunda, mafuta ya kula, maziwa na nyama nyekundu

Kabla ya kujiunga na SNV- Tanzania kipindi cha miaka (2001-2007) pia alifanya kazi na taasisi mbalimbali za maendeleo za kimataifa ikiwemo Enterprises Works World Wide Inc, Techno Serve na kampuni ya usindikaji chakula kama Meneja Msaidizi.

Silvanus ni mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Kilimo cha Mbogamboga na Matunda kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine na ana ujuzi wa aina tofauti ikiwemo kubuni uchangamano wa afua mbalimbali zilizounganishwa za maendeleo ya soko, kuwezesha uwekezaji wa hisa binafsi, usimamizi wa programu upande wa vitendo na kimkakati hususan katika; kupanga, usimamizi, uangalizi, uongozi, ubia, ufuatiliaji, tathmini na ujifunzaji.