- info@sagcot.co.tz
- +255(0) 22 260 1024
- Utaratibu wa Kutatua Malalamiko
- Fomu ya Usajili wa Malalamiko | Waajiriwa wa SAGCOT
- Fomu ya Usajili wa Malalamiko | Wasio Waajiriwa wa SAGCOT
- Takwimu za Malalamiko
- Maswali Yaliyoulizwa Mara Nyingi
Kuhusu Jukwaa Hili
Jukwaa la Utaratibu wa Kutatua Malalamiko la SAGCOT (SGRM) ni mfumo wa kidijitali ambao unawezesha taasisi ya SAGCOT kukusanya malalmiko ya wadau wake kutoka pande yoyote ya dunia na kwa wakati wowote. Pindi yanapopokelewa, malalamiko huwasilishwa kwenye idara husika kwa ajili ya kuthibitishwa na kufanyiwa kazi. Kila lalamiko hufuatiliwa kwa ukaribu kupitia mfumo wa uhakiki wenye namba maalumu ya kidijitali ili kuhakikisha masuala yote yameshughulikiwa ipasavyo.
Maoni:
Mrejesho utakaotupatia kuhusu ufanisi wa mfumo wetu wa kupokea na kushughulikia malalamiko utatusaidia kuboresha huduma hii muhimu kwako. Tunapenda kukutaarifu kwamba huduma hii ya kupokea na kushughulikia malalmiko inaongozwa na kanuni na taratibu ujulikano kama SGRM Flow Chart.(active link).
Zingatia: Endapo haujaridhishwa na utatuzi wa malalamiko yako kwa wakati kama ilivyoelekzwa kwenye SGRM Flow Chart, wasiliana nasi moja kwa moja kupitia namba za simu +255 (0) 22 2 60 10 24/46.
Masuala ambayo sio ya kutatuliwa kupitia mfumo huu
- Masuala ya kisiasa
- Masuala ya kisheria
- Masuala ya kibinafsi au kifamilia
- Masuala yanayokiuka sheria za Serikali ya Muungano wa Tanzania
- Maoni yaliyo jumuishi
Takwimu zaMalalamiko
Tuma malalamiko yako kupitia;
- Jukwaa la Utaratibu wa Kutatua Malalamiko linalopatikana kwenye tovuti ya SAGCOT www.sagcot.co.tz
- Anuani pepe : sgrm@sagcot.co.tz
- Simu: +255 (0)22 2601024 or 255 (0)22 2601046
- Sanduku la maoni lililopo ofisi za SAGCOT
- Tuma barua kwa Mkuu wa Idara ya Fedha na Tawala, Taasisi ya SAGCOT, Ghorofa ya 5, Jengo la Masaki Ikon, Kitalu Namba 153, S.L.P 80945, Dar es Salaam, Tanzania.
Chati ya Utatuzi wa Malalamiko ya Taasisi ya SAGCOT
Taasisi ya SAGCOT ina mfumo maalumu wa kupokea, kutathmini na kutatua malalamiko yanayohusu mradi kutoka jamii husika na wadau wote. Jedwali lifuatalo linafafanua zaidi namna mfumo huu hutekelezwa.
